01 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

KANISA NA MEDIA KATIKA KIZAZI CHA LEO

Watu tunaotaka kuwafikia wako wapi leo?

Maisha ya watu yameingia pia kwenye media.

Leo watu wanapata habari, mafunzo, burudani na mazungumzo kupitia radio, simu, WhatsApp, YouTube, video na majukwaa mengine ya kidijitali. Kanisa haliwezi kupuuza mazingira ambayo watu wanaishi na kusikiliza kila siku.

Agizo Kuu bado ni lilelile.

Wito wa kuwafikia watu kwa Injili haujabadilika. Changamoto ya Kanisa ni kutumia kwa hekima njia zilizopo katika kizazi hiki ili Injili iwafikie watu katika lugha na namna wanayoelewa.

01 / 20
02 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

UJUMBE HAUBADILIKI — NJIA ZA KUUFIKISHA ZINABADILIKA

Media kama chombo cha utume wa Kanisa

Injili ndiyo ujumbe.

Media haibadilishi Injili wala kuchukua nafasi ya Kanisa. Ni chombo kinachoweza kusaidia ujumbe wa Kristo kuvuka umbali, lugha, kizazi na baadhi ya vikwazo vya kijamii.

Kanisa linakwenda mahali watu walipo.

Mtu ambaye hajafika kwenye jengo la kanisa anaweza kusikia ujumbe kupitia radio au simu. Hapo media inaweza kufungua mlango wa mawasiliano ambao baadaye unaendelea kwa ufuatiliaji, mahusiano na kanisa la mahali.

02 / 20
03 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

MEDIA NI MLANGO, SI MWISHO WA SAFARI

Lengo si wasikilizaji tu — ni watu wanaokua katika Kristo

Kusikiliza kipindi cha Kikristo si sawa moja kwa moja na kuwa mwanafunzi wa Yesu.

Media inaweza kuleta mwitikio, lakini mwitikio unahitaji kufuatiliwa. Aliyeitikia Injili anahitaji kusaidiwa kukua, kuunganishwa na waamini wengine na, inapowezekana, kuwa sehemu ya kanisa la mahali.

MEDIA → MWITIKIO → UFUATILIAJI → KANISA LA MAHALI → UANAFUNZI → KUZIDISHA
03 / 20
04 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

PAULO ALIWAFUATA WATU MAHALI WALIPOKUWA

Utume uliingia katika mazingira halisi ya maisha ya watu

SINAGOGINI

Paulo aliingia katika mazingira ya kidini ambako watu walikusanyika kusikiliza na kujadili mambo ya Mungu. Alijadiliana nao katika sinagogi (Matendo 17:2, 17).

SOKONI

Athene, Paulo alizungumza sokoni kila siku na watu waliokuwapo (Matendo 17:17). Hakusubiri kila mtu aje katika mazingira ya kidini.

NYUMBANI

Paulo alifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba (Matendo 20:20). Nyumba zikawa maeneo ya mahusiano, mafundisho, ushirika na malezi ya karibu.

MAMLAKANI

Hata alipokuwa mbele ya watawala kama Feliksi, Festo na Agripa, Paulo alitumia nafasi iliyofunguka kutoa ushuhuda kuhusu imani yake (Matendo 24–26).

KANUNI: KUPELEKA UJUMBE MAHALI WATU WALIPO
04 / 20
05 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

HABARI MAALUM IPO KWA AJILI YA NINI?

Media, Kanisa na Utume

Ikiwa mtu ambaye hajamjua Yesu anasikiliza HMM leo, tunataka nini kitokee baada ya kusikiliza?

HMM haitaki kuishia kwenye kipindi kizuri, wasikilizaji wengi au wafuasi wengi. Tunataka media ifungue njia ya mtu kukutana na Injili, kufuatiliwa, kumfuata Yesu na hatimaye kuwasaidia wengine kumfuata.

05 / 20
06 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

DIRA YA HMM

Dira kamili ya HMM

Jamii inayomfuata Yesu

Dira ya HMM ni kuona watu binafsi na jamii zikibadilishwa kwa kuwafikishia Injili ya Yesu Kristo katika lugha wanayoielewa, kwa namna inayofaa na yenye kueleweka, kwa kutumia media, na kuwaona wakikua kuwa wanafunzi wanaofanya wanafunzi.

Media ina nafasi gani?

Tunatumia media kuwasilisha Injili katika lugha na namna ambayo watu wanaielewa, ili kufungua safari ya uanafunzi na kuzidisha wanafunzi.

06 / 20
07 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

HMM IPO KWA AJILI YA NANI?

Watu ambao hawajafikiwa kwa namna yenye maana + Kizazi kipya cha mjini

Watu ambao bado hawajafikiwa kwa maana yenyewe

Wanaweza kuwa karibu nasi lakini lugha, utamaduni, dini, kizazi au mazingira yao yanawafanya wasipate njia ya maana ya kuipokea na kuielewa Injili.

Kizazi kipya cha mjini

Vijana wako kwenye simu, video na majukwaa ya kidijitali. Utume si kuwalaumu kwa kuwa huko; ni kuuliza jinsi Injili inaweza kuwafikia huko kwa namna wanayoielewa.

07 / 20
08 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

NGUZO TATU ZA HMM

NANI? (WHO?) • VIPI? (HOW?) • KUELEKEA WAPI? (TOWARD WHAT?)
NANI?

WATU WASIOFIKIWA

Tunatambua watu tunaotaka kuwafikia na vikwazo zinazowazuia.

VIPI?

MEDIA

Radio, video na maudhui ya kidijitali vinafungua njia ya kuwafikia watu na kuanzisha mawasiliano na mazungumzo.

KUELEKEA WAPI?

SAFARI YA UANAFUNZI (DISCIPLE JOURNEY)

Mwitikio unaunganishwa na ufuatiliaji, Maandiko, uanafunzi na kuzidisha wanafunzi.

08 / 20
09 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

MEDIA NI CHOMBO, SI MWISHO WA SAFARI

Kutoka Media hadi Harakati ya Wanafunzi

Radio ni chombo. Studio ni chombo. Social media ni chombo. Teknolojia ni chombo.

Thamani yake ya kiutume inaonekana inaposaidia kufungua njia ya kuwafikia, kujenga uaminifu, kuanzisha mazungumzo, kusambaza Maandiko na kuunganisha mwitikio na ufuatiliaji.

MEDIA → MWITIKIO → UFUATILIAJI → UANAFUNZI
09 / 20
10 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

“KWA LUGHA WANAYOELEWA”

Kuwasilisha Injili kwa mazingira ya walengwa
A

Lugha

Maneno yanayotumika lazima yaeleweke na walengwa.

B

Utamaduni & mtazamo wa maisha na imani

Tunaelewa namna mtu anavyoona maisha, imani, familia na jamii.

C

Kizazi

Vijana na watu wazima hawatumii media kwa namna ileile.

D

Njia ya media na namna ya uwasilishaji

Chombo kinachaguliwa kwa kuangalia walengwa, si kwa sababu tu teknolojia ipo.

10 / 20
11 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

BAADA YA MTU KUITIKIA, NINI KINAFUATA?

Hapo ndipo Follow-up inakuwa muhimu

Media imefungua mlango.

Mtu anapiga simu, anatuma ujumbe wa WhatsApp, anaomba maombi au anauliza swali. Hapo mawasiliano na uhusiano vinaweza kuanza.

Huduma inaendelea.

Ufuatiliaji (follow-up) unasaidia mwitikio kuwa mazungumzo, mazungumzo kuingia kwenye Maandiko, na mtu kupata njia ya kuendelea katika uanafunzi na kuunganishwa na kanisa la mahali.

11 / 20
12 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

HARAKATI YA KUFANYA WANAFUNZI (DMM) — KWA UFUPI

HMM DMM

DMM si programu nyingine ya HMM.

Ni namna ya kufikiria matokeo tunayoyatafuta: mwanafunzi anayekua, anatii Neno, anawafikia wengine na kusaidia kizazi kingine cha wanafunzi kuanza.

MWANAFUNZI → ANAYEFANYA WANAFUNZI → KUNDI JIPYA → VIONGOZI → KANISA → KUZIDISHA
12 / 20
13 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

SAFARI YA UANAFUNZI (DISCIPLE JOURNEY)

Misingi inayoelekeza safari

Maombi + Timu

Tunamtegemea Mungu na kufanya huduma pamoja.

Upendo kwa Vitendo

Upendo wa Kristo unaonekana katika namna tunavyowajali watu.

Watu wa Amani

Watu walio tayari kusikiliza na kuitikia wanaweza kufungua njia ya kuwafikia familia, marafiki na watu wengine katika mahusiano yao ya kawaida.

Makundi ya Asili

Injili inaingia katika familia, marafiki na makundi ya kawaida ambayo tayari yapo.

DBS + Viongozi

Watu wanagundua Maandiko, wanatii, wanashiriki na viongozi wa ndani wanainuka.

Makanisa + Kuzidisha

Wanafunzi, makundi, viongozi na makanisa wanawafikia na kuwawezesha wengine.

13 / 20
14 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

DBS — KUJIFUNZA BIBLIA KWA KUGUNDUA (DISCOVERY BIBLE STUDY)

Rahisi • Inalenga kutii • Inaweza kurudiwa na wengine
1

ANGALIA NYUMA

Tulitii nini? Tulishiriki na nani?

2

ANGALIA JUU — KWENYE NENO

Maandiko yanasema nini kuhusu Mungu, watu na maisha yetu?

3

ANGALIA MBELE

Nitatii nini, nitabadilisha nini, na nitashirikisha nani?

14 / 20
15 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

MFANO: KUTOKA MSIKILIZAJI WA RADIO HADI KUZIDISHA

Hivi ndivyo hatua zinavyoweza kuungana

1. Maudhui

Programu inalenga jamii maalum.

2. Mwitikio

Msikilizaji anapiga simu au anatuma ujumbe wa WhatsApp.

3. Ufuatiliaji

Mawasiliano na uhusiano vinaanza.

4. Kundi la kawaida

Familia au marafiki wanaanza kushirikishwa.

5. DBS

Maandiko, utii na kukua katika uanafunzi.

6. Kuzidisha

Makundi mapya na viongozi wa ndani wanaibuka.

15 / 20
16 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

KANISA LINAINGIA WAPI?

Utume mmoja, nguvu tofauti

HMM inaleta nini?

Uwezo wa media kuwafikia watu, utengenezaji wa maudhui, ufuatiliaji wa walioitikia Injili, mafunzo ya DMM/DBS na uwezo wa kuanzisha mawasiliano hata na watu ambao hawajaanza kushiriki kanisani.

Kanisa linaleta nini?

Kanisa la mahali linawapokea na kuwaunganisha walioitikia Injili katika ushirika wa waamini, huduma ya kichungaji, mafundisho, uanafunzi na ukuaji wa kiroho. Hivyo mtu aliyefikiwa kupitia media hapaswi kubaki msikilizaji tu; anaweza kuwa sehemu hai ya kanisa la mahali.

HMM INAWAFIKIA WATU KWA MEDIA → WALIOITIKIA WANAFUATILIWA → WANAUNGANISHWA NA KANISA LA MAHALI → WANAKUA KATIKA UANAFUNZI → WANAWAFIKIA WENGINE
16 / 20
17 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

KANISA LINAWEZA KUFAIDIKAJE?

HMM kama mshirika wa utume

Kuwafikia Watu

Kufikiria na kuwafikia watu ambao hawafiki kwenye ibada za kawaida.

Mafunzo

Kujifunza kutumia media kwa kusudi la kiutume na kutumia misingi ya DMM/DBS katika mazingira ya kanisa.

Maudhui na Ufuatiliaji

Kutumia maudhui na njia za ufuatiliaji kuwasaidia walioitikia Injili kuendelea na kuunganishwa na kanisa la mahali.

Familia na Vijana

Kufungua mazungumzo ya uanafunzi nyumbani na kuwafikia vijana katika mazingira ya kidijitali.

17 / 20
18 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

SWALI KWA MCHUNGAJI

Eneo lako la utume liko wapi?

Ni watu gani katika eneo lako ambao hawataingia katika ibada yako ya Jumapili?

Huenda ni vijana, jamii ya Waislamu, jamii ya kabila fulani, familia ambazo hazina ushirika wa karibu na kanisa au kizazi cha kidijitali.

HMM inaweza kushirikiana nawe.

Nani hajafikiwa? Kikwazo ni kipi? Ni media gani inaweza kufungua mlango? Mwitikio utafuatiliwaje? Mtu huyo ataunganishwaje na kanisa la mahali na kukua katika uanafunzi?

18 / 20
19 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

HMM SI RADIO TU

HMM ni huduma ya media yenye utume

Siyo tu...

kutengeneza programu, kuongeza wasikilizaji, kupata watazamaji, wafuasi wa mitandao au eneo kubwa la matangazo.

Tunachotafuta...

watu kufikiwa, kuelewa Injili, kuitikia, kufuatiliwa, kukutana na Neno, kumfuata Yesu na kuwafikia wengine.

19 / 20
20 HMM • HABARI MAALUM MEDIA

HMM DMM

KUTOKA MEDIA HADI HARAKATI YA WANAFUNZI
HMM → DMM

MEDIA INAFUNGUA MLANGO.
KANISA LINASAIDIA SAFARI KUENDELEA.
WANAFUNZI WANAFANYA WANAFUNZI.

JAMII INAYOMFUATA YESU
Dira yetu ni kuona watu binafsi na jamii zikibadilishwa kwa Injili ya Yesu Kristo — katika lugha wanayoielewa, kwa kutumia media, na kuwa wanafunzi wanaofanya wanafunzi.